Patanisho: Jombi aapa kutopiga bibi yake

Edwin, 32, alipiga simu katika kipindi kinachoruka kinachopendwa na watu wengi kila asubuhi katika redio Jambo cha Patanisho kupata suluhu la takribani miezi tatu kufikia sasa. Bwana huyu alisimulia mwanzo mwisho masaibu yaliyoikumba ndoa yake ya miaka kumi na mwili. Balaa iligumbika na kuyafanya mapenzi yake kuwa shubiri kuanzia mwezi wa kwanza alipompiga mpenzi wake Christine.

Kupitia kwa njia ya kupiga simu redioni jombi huyu alionekana kusononeka sana na kuyakubali makosa yake ya kumpiga na kumdhalilisha mkewe kadamnasi ya watu “…Makosa yalitokea lakini najuta sana.Am the one who messed up… nilipiga bibi akaenda Am missing my family… mimi ndo nilijiletea shida mwenyewe.”

Baada ya kuipoteza kazi yake iliyomletea fedha za kuisetiri familia yake. Edwin alianza kupandwa na hasira za mkizi na kuanza kuivuruga familia yake kila mara. Alikuja nyumbani siku moja na kuchukua simu ya mke wake na kuanza kuipekua katika kasha la jumbe.Ujumbe aliokutana nao ukiwa wa mwanaume mteja wake Chrisine.

Baada ya mtangazaji aliyobobea katika taaluma hii Gidi kumpigia mke wake, mama huyu wa watoto wawili alionekana kutotaka kurudi katika ndoa ya vita kila mara. Alifunguka zaidi jinsi bwana huyu anawatesa yeye na watoto “Amekuwa ananifukuza kwa nyumba, kunipiga pamoja na watoto mara anatupa anatupa vitu nje ya nyumba.”

Kwa majonzi zaidi amesimulia jinsi na ambavyo ndoa hii ya miaka kumi na miwili ilikumbwa na tandabelua na zogo tele. Bibi huyu alihoji kuwa jumbe zilizokuwa katika simu zilikuwa za mteja wake wa kiume na walikosana na bwanake. ”Huyo mtu alimtext nasty words na kuanza kunipiga mbele ya mamake…ata mbele ya wazazi wake wote”

Christine alifunguka jinsi bwanake anamshuku kila mara na wanaume na ata kufikia kiwango cha kuwakana watoto .“Unasema watoto si wako… you almost killed me mbele ya watu wengi .Give me time …” alifoka Christine.

Bibi yake amesema yupo radhi kurejea katika ule uhusiano iwapo atabadilika na kuasi tabia za kinyama na kumdhalilisha. ” If I hear changes from people I will come back.”

Patanisho hii ilifikia kikomo na Gidi kumtaka Edwin kula kiapo kwa kuinua mkono wake wa kulia “..Mimi Edwin Odero naapa ya kwamba sitarudia tena kumpiga mke wangu mama Beverly, kumwaibisha mbele ya familia na nitampenda kuanzia leo hadi kifo kitutenganishe Amina”