PATANISHO: Bwanangu huchukua simu yangu na kwenda nayo kazini

Gidi na Ghost Patanisho
Gidi na Ghost Patanisho
Lora alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bwana George.
"Nilikosana naye mwezi wa nne kwani nilipokuwa kwake wafanyikazi wenzangu walinipigia simu na nilipotoka nje kupokea simu, alidhani ni mpango wa kando na akanifukuza." Alieleza Lora akidai kuwa mumewe humshuku.

Isitoshe bwanake hubeba simu yake na kwenda nayo kazini mwake kwani humshuku yeye hushinda akizungumza na wanaume wengine.

Wawili hao wamejaliwa watoto mapacha katika ndoa ya miaka mitatu.

Alipopigiwa simu bwana George aliuliza; "Sasa wewe unaenda na watoto wangu twins nyumbani na ni wewe una makosa? Kama ni makosa nataka watu wawili kutoka kwenyu na wawili kutoka kwetu ili tuombane msamaha?"

Itakuwaje mimi nikipiga simu hujibu ukiwa hapo lakini wewe zako huwa unajibu nje na unafuta nambari kwa simu?" Aliuliza George.

Hiyo siku nilikuwa naosha vyomba na jirani yangu alikuwa anapita hapo na sufuria ikaanguka, sasa mume wangu akashuku nilikuwa na uhusiano naye. Alijitetea Lora.