Idadi ya watu waliofariki katika ajali za barabarani kuanzia jana jioni sasa imefikia watu 14 baada ya ajali nyingine kutokea mapema leo huko matulo kwenye barabara ya Eldoret kwenda Malaba .Ajali hiyo ilitokea wakati matatu iliyokuwa imewabeba abiria kugonga trela ambalo lilikuwa limeegeshwa kando ya barabara .
Kamanda wa traffic Bungoma mashariki Rodgers Lwembe amesema sita waliojeruhiwa wanapokea matibabu katika hospital ya kaunti ya webuye.
Jana usiku ajali nyingine kwenye barabara ya malindi kwenda Mombasa ilisababisha vifo vya watu saba . Ajali hiyo ilitokea wakati gurudumu la trela moja lilipopasuka na kulifanya kugonga matatu ya abiria .