Mwalimu auawa ,Polisi 2 wajeruhiwa katika shambulzi la majangili Turkana

Mwalimu  mmoja wa shule ya msingi  ameuawa kwa kupigwa risasi ilhali maafisa wawili wa polisi wa utawala  wamejeruhiwa baada ya gari la polisi kushambuliwa na majangili  huko Turkana mashariki .kamanda wa polisi wa kautni ya Turkana  Samuel Ndanyi  amesema gari hilo la polisi lilikuwa likielekea katika kituo cha kibiashara cha  Lokori kutoka Napeiton .

Shambulizi hilo lilitokea mwendo wa saa tatu unusu asubuhi . Mwalimu  aliyeuawa ametambuliwa kama  Oscar Keya  ambaye alikuwa katika likizo ya katikati ya muhula  na alikuwa ametumia usafairi wa gari hilo la polisi kwa sababu eneo hilo halina  huduma za usafiri wa umma  kwa ajili ya hali mbaya ya usalama na ubovu wa barabara .

Kamanada huyo wa polisi wa kaunti amesema maafisa wa  GSU na RDU tayari wametumwa  katika eneo hilo kuwasaka majangili waliotekeleza shambulizi hilo