NA ABRAHAM KIVUVA
Kituo chako mahabubu cha Redio Jambo kimeratibisha mchakato na mpango mzima wa kuwatunuku wasikilizaji na mashabiki sugu kwa zawadi kemkem mwezi huu wa Julai na Agosti.
Pia soma:
Kupitia swali mboga sana la kuitambua “the phrase that pays”, msikilizaji anatuzwa shilingi elfu moja. Kwa kutengeneza bango na kuandika radio jambo ongea usikike, mshindi anatuzwa elfu 5 pesa taslimu.
Mashabiki wa kutoka sehemu za ukambani na maeneo ya Taita taveta watapata nafasi adimu zaidi kuonana macho kwa macho na sonko wa radio Jambo juma lijalo.