Tume ya kuwaajiri walimu TSC imesitisha nyongeza ya mishahaya ya walimu 103,624 ambao ni wanachama wa muungano wa KNUT .TSC imesema nyongeza hiyo ya malipo haikujumuishwa katika awamu ya tatu ya mkataba wa CBA wa 2017-2021 baada ya mahakama kuamua kwamba masharti hayo yategemee mikataba ya utendakazi na sio mwongozo wa ustawi wa taaluma za walimu hao kama ilivyotaka TSC .
TSC imesema kwa sababu ya uamuzi huo ,haingeweza kutekeleza nyomngeza hiyo ya malipo chini ya awamu ya tatu ya kutekeleza makubaliano ya CBA . Walimu watakaoathiriwa ni pamoja na walimu wakuu , manaibu wao na walimu waandamizi . Mzozo kati ya TSC na KNUT kuhusu mikataba ya utendakazi ,kuajiriwa kwa mikataba ,uhamisho wa walimu ,kupandishwa vyeo kwa walimu na ustawi w ataaluma zao ulifikihswa kortini baada ya TSC kuushtaki muungano wa KNUT ili kuzuia mgomo wa walimu .