- Sonko amekanusha kujihusiaha na ufisadi
- EACC ilizifuata pesa hizo hadi katika Akaunti yake
- Sonko amesema zilikuwa za biashara kabla hajaingia City Hall
Gavana wa Nairobi Mike Sonko amesema shilingi milioni 20 zilizopatikana katika akaunti yake na maafisa wa EACC zilikuwa za biashara alizofanya kabla ya kuwa gavana wa Jiji. Gavana huyo ameshtumiwa kwa kupokea rushwa ya shilingi milioni 20 kutoka kwa kandarasi yenye kiasi kikubwa cha pesa ya ukusanyaji taka jiji katika miaka ya kifedha ya 2017-18 ba 2018-2019. Tume ya EACC imedai kwamba baadhi ya kampuni zilizoshinda zabuni hiyo ya shilingi milioni 357 zilihamisha kwa akaunti ya Sonko zaidi ya shilingi milioni 20 .
Sonko hata hivyo ameyakanusha madai hayo akisema kamwe hajajihusisha na ufisadi . Pia ameongeza kwamba kaunti ya Nairobi imelipa kodi zote isopokuwa kiasi kilichorithiwa kutoka kwa uatawala wa gavana wa zamani Evans Kidero .Sonko amesema kaunti ya Nairobi imelipa zaidi ya shilingi bilioni tano kama ushuru .
Pia kaunti ya jiji haijatoa shilingi milioni 5o zinazofaa kuwalipa wafanyikazi wa jiji mishahara yao ya mwezi huu. Gavana huyo alihojiwa siku ya jumanne kwa zaidi ya saa nane katika makao makuu ya EACC na kurekodi zaidi ya taarifa 13 tofauti .