PATANISHO: Mke wangu akirudi lazima tuongeze watoto wawili

Victor alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Melvine, ambaye walikosana na akaondoka na kumuachia watoto.

"Sasa unajua nilimpiga nikiwa mlevi kwani nilikuwa nimempea pesa akanunue mboga na kuingia kwa nyumba nikapata amenunua skuma. Kwa hali ya ulevi kulitokea kisirani kidogo na nikampiga. Hapo alikasirika na kwenda na sasa ni zaidi ya miaka mitatu." Alisimulia bwana Victor.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka kumi na miwili na kisa hicho kimemfanya bwana Victor kuwacha pombe.

Kulingana na Victor wanawe wanaishi na babake nyumbani na kulingana na utafiti wake mkewe bado hajaolewa. Juhudi zake za kumbembeleza mkewe arudi hazijafua dafu.

"Siku moja alinidanganya atakuja na hadi nikafanya budget ya kupika kuku na kupanga nyumba lakini nilingoja mgeni ambaye hakuja." Aliongeza Victor.

"Unajua alikuwa anakunywa pombe sana na nikaamua kutoka na kuwacha watoto wawili lakini niko. Sasa inafaa tuongee tuelewane halafu ndio nirudi." Alisema bi Melvine.

Mimi niko tu na wewe lakini wacha pombe kabisa ili nirudie watoto. Kama uliwacha nitarudi juu siwezi wacha watoto wangu wahangaike ama unaonaje? Melvine aliuliza mumewe Victor huku akimhakikishia kuwa atarudi kwani alikuwa anaishi na dadake.

Bwana Mulee alimuapisha bwana Victor ambaye alikiri kuwa katu hatompiga mkewe wala kunywa pombe tena maishani mwake. Wapendwa hao wawili walisameheana na kudai kuwa watafanya mipango waongeze watoto wawili.