Akothee gizani huku bintiye Rue akifaulu katika shindano la Miss Universe Kenya

rue1
rue1

Rue binti yake Akothee ana matumaini ya kuwa mshindi kwenye mashindano ya Miss Universe Kenya.

Rue alisema kuwa, kujikaza kisabuni, kutunza wakati na unyenyekevu ndivyo vitu ambavyo vimemfanya aweze kufika aliko sasa.

Hata hivyo, amini usiamini binti huyu hajampa mama yake habari hizo na hata hakuwa amemwambia mama yake alipojiandikisha kwenye mashindano hayo ya Miss Universe Kenya.

.

Akizungumza na vyombo vya habari, Rue Baby alisema kuwa, bado hajampa mama yake uhondo na mama yake ata hakuwa anajua kinachoendelea kwani hakujua kama anaweza fika alipofika sasa.

Vilevile, Rue alisema kuwa anasubiri siku nzuri tu ambapo ataketi chini na mama yake na kumpa habari nzuri.

"Actually my mother doesn't know about this. I didn't tell her because I didn't know I was going to make it this far. I am waiting for a good day, when I'll sit her down and tell her that I've made it to this point."

Licha ya hayo, Rue aliwaambia mashabiki wanaomwonea kwenye mitandoa ya kijamii kuwa, wasidhani kufika kule alipo kumekuwa rahisi sana kwani ilimbidi achume juani kwa muda mrefu ili aweze kufika alipo sasa.

Vilevile, alisema kuwa hata mama yake mzazi hakujua kama ako kwenye mashindano hayo na kwa hivyo, mama yake hakuchangia hata kidogo kumsaidia kufika alipofika sasa.

"I have seen many negative comments, saying that it's my mother that got me into the competition. I have worked myself so hard and I'm also very competitive to get the crown. It is my hard work that has gotten me there. You see now my mother doesn't even know about this," Rue alisema.

Rue alizidi kusema kuwa alikuwa amekumbwa na matatizo mengi sana na kama mama yake angekuwa anamsaidia basi hangekuwa amekumbana na majanga yaliyompata

"If I had it easy, then I don't think I'd have conquered the challenges. I don't have it easy. It's very hard on my side. I have to go all out and be outstanding.''

Hata hivyo, Rue alisema kuwa, mama yake amekuwa akimsaidia sana akiwa kwenye kiwanda chake cha urembo na ana uhakika kuwa, mama yake atafurahi sana pindi tu atampa habari hizo.

"She will be very happy when I tell her the news."Rue alisema.