Habari Muhimu Toleo la saa Kumi Jumanne 15/10/2019

RADIO JAMBO MIC
RADIO JAMBO MIC
Inspekta  mkuu wa polisi Hillary Mutyambai ameagizwa kuanzisha uchunguzi  kuhusu madai ya   vitendo vinavyokiuka sheria na uhalifu  katika idara ya uhamiaji . Hii ni baada ya ufichuzi uliotolewa katika runinga ya Citizen  kuhusu njama ya maafisa wa polisi na wale kutoka idara hiyo kutumia vitisho  vya kumfurusha nchini mfanyibiasha mmoja wa asili ya kiasia ili kuichukua mali yake . msemaji wa wizara ya usalama wa ndani Wangui Muchiri amesema  Mutyambai anatakiwa kuwasilisha ripoti ya  hali ya uchunguzi wake ndani ya kipindi cha siku 14 .

Mbunge wa Tiaty William Kamket  amewashtumu polisi kwa kutochukua hatua za kumtafuta mwanafunzi wa chuo kikuu aliyetekwa nyara katika kituo cha kawi ya mvuke cha olkaria ambapo alikuwa akifanya masomo ya kujifunza kazi . Kamket amesema mwanafunzi huyo alitoweka jana usiku  mjini Naivasha wakati alipokuwa akiburudika na wenzake na amemshtumu OCPD WA eneo hilo kwa kujikokota katika jitihada za kuwakamata washukiwa .

Upo katika hatari ya kuhusika katika ajali ya barabarani siku za ijumaa ,jumamosi na jumapili kuliko siku yoyote ya wiki .Takwimu za NTSA ZAONYESHA KWAMBA  watu zaidi ya 400  waliaga dunia katika ajali zilizotokea katika siku hizo  kati ya januri na oktoba . watu 500 waliaga dunia siku za jumapili ,480 siku ya jumamosi ilhali 406 waliaga dunia siku za ijumaa .

Shirika la feri  limeikabidhi familia ya  marehemu Mariam Kighenda shilingi laki mbili  ili kuisaidia familia yake kwa  matayarisho ya maazishi yake na bintiye Amanda Mutheu  . mumewe Mariam , JoHN WAMBUA PIA amepokea hundi ya shilingi elfu 682,500 kutoka kwa kampuni ya bima  kwa gari lao lilitumbukia baharini  na familia yake

Kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi amewaomba waajiri kuwaruhusu wafanyikazi wao wanaoishi Kibra  kushiriki uchaguzi wa Novemba tarehe saba .Mudavadi amesema  wenyeji wana wajibu wa kumchagua kiongozi ataayekamilisha kazi nzuri iliyoanzishwa na marehemu Ken Okoth .

Mzozo  kati ya serikali na madreva wa magari ya mizigo unaendelea licha ya serikali kusema kwamba iliondoa agizo lililohitaji mizgo yote kusafirishwa kwa  reli ya SGR .mfanyibiashara salim karama amesema hakuna kampuni ya uchukuzi iliyorejelea oparesheni zake .