Aisha Jumwa awavamia Kingi,Joho na Raila Odinga kwa maneno

YjUn7SygspFB_IMG_1551444835093
YjUn7SygspFB_IMG_1551444835093
Kovu la mauaji Ganda linaonekana kupoa. Tukio hilo lilichafua jina la Aisha Jumwa baada ya kuhusishwa na kupelekea kukamatwa na wanapolisi.

Mbunge wa eneo bunge la Malindi Aisha Jumwa sasa amewajia juu na kuwavamia magavana Kingi na Joho kwa ukali.

Huku akisema wawili hawa wanaabudu Raila Odingaa, Jumwa ametaja usaliti mnene wa magavana hawa kwa waliowachagua.

Jumwa anapima kupata kiti cha ugavana Kilifi uchaguzi wa 2022.

 Aidha, Jumwa ana madai kuwa Raila Odinga anawatumia vibaya wakaazi wa mikoa ya pwani.

Jumwa alitangaza kuunga mkono naibu wa rais William Ruto.

https://twitter.com/HonJumwa/status/1190354987420966913

Mama huyu aliasi chama chake cha ODM na kupigwa vita zaidi nyakati za hapo awali.

"Hamna uongozi Kilifi unaojali maslahi ya watu. Anachofanya Kingi na timu yake ni kuabudu chama na mtu mmoja. Hawajali watu ambao sasa ni maskini wakubwa," Jumwa alifoka.

Alimkashifu Kingi kwa kuzidi kuabudu Raila Odinga,

"Tumemuunga mkono Raila kwa miaka 15 na hatujapa kitu. Tuliahidiwa kiti EALA lakini kiti hicho kilipewa Oburu Odinga, Kingi anajua hili lakini amekimya. Anamwabudu mtu mmoja na chama. Aibu gani hii Kingi, aibu gani Kingi,"Jumwa