Itakuaje? Idah Odinga na Lwam Bekele wapewa wiki mbili kusuluhisha kesi

ida
ida
Korti ya juu zaidi ya Kenya imewapa Ida Odinga na Lwam Bekele wiki mbili ili kusuluhisha kesi ya mali yake Fidel Odinga.

Wakili wake Lwam, bwana Roger Sagana aliiambia mahakama kuwa wamekuwa na mikutano mbali mbali lakini bado mpaka sasa hawajaweza kusuluhisha tatizo hili.

Wakili wake Lwam, Roger Sagana alisema kuwa anaomba apewe wiki mbili ili aweze kusuluhisha kesi ile.

Vilevile, Phoebe Gweno mwanamke anyesemekana kuwa mama ya watoto wa Fidel ambao ni mapacha alihusishwa katika kesi hii.

Mapacha hawa wanafaa kupimwa ili korti iweze kudhihirisha kuwa mapacha hawa ni watoto wa Fidel.

Hakimu Aggrey aliamuru kuwa kesi ile itajwe Novemba tarehe 27.

Familia ya Raila pamoja na Lwam imetatizwa sana na vile ambavyo watagawa mali ya Fidel.

Katika karatasi za korti, Idah na binti yake Winnie walitoa sababu nyingi sana za kumfanya Lwam asiwe mmiliki halali wa mali ya Fidel.

Zaidi ya hayo, Lwam alisema kuwa hana tatizo kamwe kuwakubali mapacha wale miongoni mwa watakao rithi mali endapo majibu ya mapacha wale yatatokea na iwe wazi bayana kuwa watoto wale ni watoto wa marehemu Fidel.

Fauka ya hayo, korti ilikataa madai ya eti kesi iwe siri kwani kesi ikifika kortini haiwezi kuwa siri tena, hata hivyo, korti iliamuru vyombo vya habari kuficha majina ya watoto ili wawaepushe na mambo ya watu wengi.