Jowie kusalia tena gerezani Krismasi hii, hatma ya kesi yake kubainika mwakani

Jowie
Jowie
Joseph Irungu maarufu kama Jowie atasalia kuzuizini Krismasi hii kwa mara ya pili tangu kukamatwa kwake huku akisubiri korti iamue kuhusu ombi lake la kuachiliwa kwa dhamana mnamo Februari 13, 2020.

Jowie alikamatwa Septemba 25 mwaka uliopita na Krismasi mwaka huo ikampata kwenye rumande.

Mnamo Juni 18, 2019, mahakama kuu ilikataa kumpa dhamana Jowie kwa mara ya pili.

Jaji James Wakiaga alifutilia mbali ombi la Irungu la kuachiliwa kwa dhamana kwa madai kuwa kesi haikuwa imeskizwa na pia hakukuwa na ithibati tosha.

Aidha, Jaji huyo aliagiza mashahidi wote watoe ushahidi wao kortini kabla ya kuamua iwapo atamwachilia Irungu kwa dhamana.

Jowie alikuwa anataka ombi la kuachiliwa kwa dhamana, ambalo alikuwa ametuma awali litathminiwa upya, ila jaji alikataa huku akisema ni yeye ni hatari kwa usalama.

Mashtaka ya mauaji yanayomkabili yeye na Maribe yatarejelewa Machi 2020.

Hata hivyo mfanyakazi wa nyumbani wa Maribe alitoa ushahidi kortini kwamba usiku moja Jowie alijipiga risasi.

Pamela Kembo pia alieleza korti kuwa Jowie alikuwa akimpeleka Maribe kazini na kumrejesha kama desturi kulala.

Aidha alieleza mahakama kuwa Maribe alimjulisha kuwa Jowie hufanya katika Ikulu.

Alipokuwa kwa makaazi ya Maribe, Kembo alisimulia kuwa kwa wakati moja aliona bunduki na akaambiwa kuwa ni ya Jowie.