Amepata mpenzi? Maribe asherehekea birthday na busu moto! (Video)

Hii leo ikiwa siku yake ya kuzaliwa, mwanahabari Jacque Maribe tayari alianza sherehe zake kwa njia kuu.

Maribe pamoja na rafiki yake wa dhati Chemutai Goin na Angela Cheror, Jacque alipiga sherehe katika klabu moja ili kujipa usiku wa furaha tele.

Jacque kupitia mtandao wake wa Instagram aliandika,

“ABOUT TO USHER IN THIS BIRTHDAY WITH BFF,” AKIONGEZA, “BIRTHDAY WITH GIRLS.”

Hili laja miaka kadhaa tu baada yake na marafiki wake wa dhati Terryanne Chebet, Shix Kapienga, Monicah Kiragu na Kirigo Ngarua, kuwaacha wengi na hamu kuu ya kuwa na marafiki wa hadhi kama ile.

Kama ulikosa basi tizama picha ya Jacque aliposherehekea siku ya kuzaliwa na marafiki hao.

Hata hivyo mambo hubadilika na ni dhahiri kuwa tayari amebadilisha marafiki wake na hawa ndio walioko katika kundi la marafiki wake.

Kando na hilo, kilichowavutia wengi ni jamaa asiyejulikana aliye rekodiwa akimbusu Maribe na kusakata naye densi usiku uliopita.

Tazama kanda ifuatayo uone jinsi alivyokaribisha birthday yake jana usiku.