Joyce Laboso angeletwa kwangu angepona ugonjwa wa saratani, asema James Ng'ang'a

pastor-James-Nganga-715x405-696x394
pastor-James-Nganga-715x405-696x394
Kasisi wa kanisa la Neno Evangelism Center amefunguka kuwa ana uwezo wa kuponya wa saratani.

Katika mahubiri kanisani, Ng'anga alisema iwapo marehemu Joyce Laboso angeletwa kanisani mwake angemsaidia na kumponya makali ya ugonjwa huu wa kansa.

Ng'ang'a amesema kuwa maombi na imani ndio miundomisingi ya kumponya mgonjwa yeyote.

Muhubiri huyu amenukuliwa katika vyombo vya habari kwa kuzingirwa na utata mwingi.

Akihojiwa katika kituo hiki hapo awali, muhubiri huyu alifungukia Massawe jinsi anavyokerwa na wanaomchamba na kumkejeli kwenye mitandao ya kijamii.

“Huwa nafanya mambo mengi mazuri. Nawapa watu chakula, lakini hao wanakata tu (video)  ile nimeongea vibaya kwa sababu ni watu wana mapepo." Alisema Ng'ang'a.

Ng’ang’a alikana taarifa za kutamani kujiua.

"Niliskia taarifa kuwa kuna watu wanasema kwamba waliniona nikiendesha V8 nikiwa na mawazo, ni kama nataka kujia."

"Hebu tuwe wakweli. Mbona nijiue? Angalia bibi wangu mrembo. Nitamwachia nani nikijiua." alijitetea Ng'ang'a

"Nitaachia nani magari yangu na jumba langu. Labda niwafahamishe majirani zangu ni wazungu. We just say ‘hi’ to each other, hakuna mambo ya kushinda tukibishania mlango.." Aliendelea kujinadi

Aliwaonya mahasidi wake wakome kueneza taarifa za uongo kuhusu ibada zake.