Wanaume mashuhuri wanaojivunia kuwa wazazi

Watoto ni baraka na huwa nafurahishwa sana endapo wanaume wanajivunia kuwa na watoto wao kwani ni wengi si kidogo ambao hutengana na mama ya mtoto wao na hata kusahau kabisa kama ana mtoto na mtoto huyo anafaa kushughulikiwa.

Hivyo basi, radio jambo iliamua kuorodhesha wanaume ambao huonyesha wazi wanavyojivunia watoto wao.

Tazama orodha hii.

1.Mbusii

Presenta wa Radio Jambo, Mbusi ni jamaa freshi sana ambaye anapenda familia yake.

Mbusi ana mke mmoja na watoto watatu.

https://www.instagram.com/p/B3eIsp1pPYu/

https://www.instagram.com/p/B2Nw1UUnSIp/

Juzi ilikuwa siku ya kuzaliwa kwa mtoto wake na ni wazi bayana kuwa ana furaha kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mtoto wake kwani aliweka picha ya mtoto wake kwenye mtandao wa kijamii na kuandika ujumbe mtamu sana.

2. Mariga

Mariga ni mwanakandanda ambaye amegeuka na kuwa mwanasiasa kwa sasa ana mtoto mmoja wa kike.

Amini usiamini, kitoto chake Mariga ni mrembo si kidogo.

Mgombeaji wa kiti cha ubunge huyu, huweka picha zake na za mtoto wake kwenye mitandao ya kijamii na hivyo basi, tunaweza kudhibitisha kuwa anajivunia mtoto  wake sana.

3. Gidi

Gidi ni presenta wa show ya Gidi na Ghost asubuhi na kitengo maarufu cha Patanisho, na ni wazi kuwa mapenzi yake kwa watoto wake na familia yake haiwezi fifia.

https://www.instagram.com/p/B28R7csgF-9/

https://www.instagram.com/p/B2BWEYag_eS/

4.Njugush

Njugush ni mcheshi aliyetajika sana nchini.

https://www.instagram.com/p/Bz7ONLwnwWK/

https://www.instagram.com/p/B1yJXVXntYv/

Jamaa huyu ana bibi na mtoto mmoja wa kiume ampendaye sana.

5.Nameless

Mwanamziki Nameless ni jamaa ambaye ni wazi belua kuwa mapenzi ya familia yake ni ya kweli kwani jamaa huyu huandika ujumbe mtamu kila wakati awekapo picha ya mtoto wake kwenye mtandao wa kijamii.

Jamaa huyu ana mke mmoja na watoto wawili wa kike.

https://www.instagram.com/p/BxUPM6zFfDy/