Mwanamke ajitia kitanzi baada ya ugomvi wa Sh100 na mumewe

Ubishi baina ya wapenzi wawili kuhusu shilingi mia moja ulimalizika vibaya baada mke kuchukua kamba na kujitia kitanzi katika mtaa wa Mithuri, Naivasha

Mama huyo wa miaka 24, aligadhabishwa na kuendea kamba baada ya mumewe kumshtumu kwa kutotumia fedha za chakula vyema.

Wakati wa tukio la Alhamisi asubuhi, mwanamke huyo na mtoto wake wa mwaka mmoja walitoka kwenye nyumba yao kwa haraka baada ya ugomvi kabla ya mwili kupatikana ukining'inia mtini.

Kulingana na OCPD wa Naivasha, Samuel Waweru, uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa hapo awali wanandoa walikuwa wakigombana kuhusu maswala kadhaa ikiwamo jinsi mwanamke huyo alikuwa akitumia pesa hizo.

Hayo yakijiri,  mazungumzo ya nyongeza ya mishahara kati ya muungano wa  walimu wa KUPPET na wizara ya elimu yataangazia zaidi maslahi ya walimu wa daraja la chini.

Katibu wa KUPPET tawi la Taita Taveta  Shedrack Mutungi anasema mazungumzo hayo pia yatajumuisha marupurupu tofauti ambayo walimu wanafaa kupata.Ansema wanalenga kuanisha mishahara ya walimu pamoja na ile wasimamizi.

-Anthony Gitonga