ILIKUAJE: Mpenzi wangu wa kwanza aliaga na kuniwachia mtoto - Sudi Boy

sudi boy
sudi boy
Sudi mohammed almaarufu, Sudi Boy, ndiye aliyezuru studio zetu leo katika kitengo cha Ilikuaje naye Massawe Japanni.

Mojawapo ya vitu alivyozungumzia ni muziki na pia familia yake huku akifichua kuwa ana watoto watoto ambao wote wana mama tofauti.

Alifichua kuwa mtoto wa kwanza sio wake ila alikuwa wa mpenzi wake wa kwanza ambaye aliaga dunia baada ya kuugua.

Mpenzi wangu wa kwanza aliaga dunia baada ya kuzidiwa na Pneumonia, na kuniwachia mtoto ambaye nalea. Watoto hao wengine wawili kila mmoja ana mamake.

Hata hivyo, Sudi anasema kuwa angependa kupata watoto wengi bora awe na uwezo wa kuwalea.

Msanii huyu wa kutoka Mombasa amekuwa katika sanaa ya muziki kwa miaka 13 sasa na anatambulika kwa ngoma kama; Nalo twende nalo, naona bado na iromo.

Hivi sasa ana wimbo mpya kwa jina kolola aliouzindua siku kadhaa zilizopita na tayari unafanya vyema katika mtandao wa Youtube.

Shida kuu aliyopitia kama msanii kutoka Mombasa?

Kujipambania ndio ngumu sana kwani unapata watu hawakubali kuwa hii ndio kazi itayowalisha na kulea watoto. Unapata mtu akizindua ngoma anatulia.

So tunafaa kutia bidii kwani ukijituma utafika unapoenda.

Kazi ingine anayofanya?

Muziki wangu ndio unanilisha mimi na watoto watatu na sina kazi nyingine ninayofanya. 

Babangu alikuwa mwanamuziki ila sikujua na nikama kuna kitu kilimfanyikia na akaamua kuwacha na hadi wa leo sijawahi jua mbona akawacha.

Sudi anasema babake alikuwa anafaa kwenda ng'ambo na ikawa shida kati yake na mamake na wenzake walienda naye akabaki. Jambo hilo lilimchukiza kwani alikuw anajua kuwa humo nje angesaidika.

Licha ya hayo Sudi anasema kuwa babake anamshikilia na kumuunga mkono.

Tazama wimbo wake 'Kolola' hapa,