Alianguka tukiwa likizoni mkewe billionea Reginald Mengi asema.

54513034_2204960783150759_2180049391568978198_n
54513034_2204960783150759_2180049391568978198_n
Mkewe billionea Reginald Mengi alisimulia kinagaubaga vile mumewe  alianguka kuaga dunia wakiwa kwenye likizo.

"Tuikuwa katika hoteli nchini Dubai imi,mume wangu na watoto,Mengi alianguka ghafla, tuliambia hoteli itutafutie hospitali bora ili tumpeleke kwa matibabu
kifungua mimba wake alikuja hospitalini na pia ndugu yake Benjamin." Jacqueline Alisimulia.

Alizidi na kueleza.

" Awali tulikuwa tumeenda nchini Zanzibar, lakini Reginald alituambia tusafiri nchini Dubai ili watoto wakajifutahishe kabla warudi shule." Alizungumza.

Baada ya kifo chake Jacqueline alilaumiwa na kuambiwa kuwa ni yeye ndiye aliyemuua Reginald Mengi.

"Baada ya kifo cha Mengi mengi yalisemwa, na kuambiwa kuwa ni mimi nilimuua, balozi wa Tanzania aliyekuwa akitusaidia kusafirisha mwili kutoka Dubai alimwambia ndugu yake Mengi kuwa ni hatari sana kusema maneno hayo

Alimwambia aambie vyombo vya habari ukweli ili watu wajue ukweli ni upi." Alieleza.

Waliporudi Tanzania Benjamin hakusema chochote jambo ambalo lilimuumiza sana, Mengi aliacha  wasia ambao ndugu yake hakufurahishwa na chenye Mengi alikuwa ameandika na kupeleka kesi mahakamani.

"Baada ya wasia kusomwa, Benjamin na mwanawe Mengi wa kwanza walikataa wasia wa bwanangu na kenda mahakamani,

Kuna utajiri mwingi kwa kila mtu wa kupata na kuishi maisha mema,na aliyetafuta utajiri huo kwa bidii yote hayupo tena na hatutaenda na utajiri wenyewe kaburini."Jacqueline Alieleza.

Jacqueline alisema kuwa anataka familia ambayo imehusika na kesi hiyo waache kusema maneno mabaya kuhusu mumewe na wawache alale salama.