Mistari ya gospel ilipotea ama? mashabiki wamuuliza Size 8

pjimage (6) (1)
pjimage (6) (1)
NA NICKSON TOSI

Msanii wa miziki ya injili Size 8 amejikuta pabaya baada ya kushirikishwa na msanii Masterpiece kwenye muziki wake mpya  High Bila Ndom ambao umetajwa kuwa hauna ujumbe wowote.

Mashabiki walidhihirisha hamaki yao kwa mwanamziki huyo, wengi wakimwambia kuwa nyimbo zake zilikuwa zinawapa moyo wengi ila kwa wimbo aliokuwa ameshirikishwa na msanii Masterpiece haukuwa na ujumbe wowote wa maana.

Wengine wakaanza kumuuliza hatua ambazo ameanza kuzichukuwa katika taaluma yake ya muziki kwani nyimbo zake za hivi karibuni  zimeanza kupoteza ladha.

Aki size 8 kwa miaka mingi umekuwa msanii bora wa nyimbo za injili ninayempenda na mshauri wamgu. Nimekuwa nikikufuatilia kwa mitandao lakini huu ulioufanya na masterpiece HAPANA, haustahili kufanya muziki kama huu, ni maoni yangu tu. Ujumbe uliondikwa na shabiki.

Kwa upande mwingine, mchumba wa Size 8 alijitokeza na kuusifia wimbo huo akisema wimbo mzuri wa injili huezi tathminiwa jinsi unavyoimba na kiwango chake bali ujumbe.

''Wimbo mzuri wa injili  huezi tathminiwa  vile unavyoimbwa ama kitengo chake bali ujumbe unaosemwa katika wimbo huo, Waefeso 5;18. Usilewe kwa divai bali  jazwa na  nguvu za roho mtakatifu''. Aliandika DJ Mo.

Wanamuziki wa nyimbo za injili wamekuwa wakiibua hisia mseto miongoni mwa wafuasi wa nyimbo hizo haswa katika ujumbe wanaoudhamiri kuutoa.

Wengine wamekuwa wakishirikiana na wanamziki wanaofanya nyimbo za kizazi kipya, hatua ambayo wengi wameiona kama ya kupotoka na kupoteza maadili.

Hapa ni baadhi ya maoni ya watu.

 Aki nafikiria hataendelea kufanya mziki wa aina hii .

 AKI SASA NDO NINI? KENYAN GOSPEL !!!!!!

 Waa hii ni gospel kweli, hata kama 😢

 Itachezwa tu si unajua mzee ndo dj!!!

 😂😂😂😂😂 Waah Aki wasanii wa injili wakenya tuwapeleke wapi?,coz vitu munaimba ata shetani anawashangaa nani anawafunza

" />