Mwanafunzi wa kidato cha tatu aaga baada ya kupata majeraha

Familia moja katika kaunti ya Busia wamebaki kwa huzuni baada ya kumpoteza mtoto wao, alipokuwa akitibiwa na kufanyiwa upasuaji baada ya kupata majeraha akicheza mchezo wa raga shuleni na timu nyingine.

Alifariki akiwa hospitali ya Eldoret, mwanafunzi huyo aliyefahamika kama Eliakim Oundo alipata majeraha hayo wakiwa wanacheza na timu mbili za raga za shule ya upili ya Sigalame na  Nambale.

Eliakim alikuwa mwanafunzi wa shule ya upili ya Sigalame

Akiongea na stesheni moja humu nchini, babake Eliakim aliwalaumu walimu kwa kutochukuwa hatua za haraka kuhusiana na kitendo hicho baada ya timu ya Nambale kuwatishia wachezaji wa Sigalame kuwaumiza.

"Baadhi ya walimu wengine waliniambia kuwa timu ya Nambale walikuwa wametishia kuumiza  na kufanyia kitendo timu ya Sigalame

Walisema kuwa ambyulensi inapaswa kuwa tayari kwa maana kuna mtu atakufa ama kuumia, najihisi kuwa usimamizi wa shule hii ungechukua hatua zaidi ili kubaini kiini cha matisho hayo

Baina ya timu hizo mbili." Alieleza.

Tukio hilo lilitokea ijumaa wiki jana,  Eliakim alipelekwa katika hospitali ya Busia na kupelekwa tena katika hospitali ya kibinafsi ya Life Care kaunti ya Bungoma.