Tanzia! Kocha wa zamani wa Western Stima Henry Omino aaga dunia

NA NICKSON TOSI

Aliyekuwa mkufunzi mkuu wa Western Stima Henry Omino ameaga dunia.

Omino alifariki mapema siku ya Ijumaa  akiwa nyumbani kwake kaunti ya Siaya baada ya kuugua kwa takriban miaka mitano akiugua saratani.

Omino ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 71 na familia yake imedhibitisha kuwa mzee huyo chini ya wiki moja iliyopita walikuwa wametafuta ufadhili wa pesa za kumpeleka kupata matibabu baaada ya hali yake ya afya kudhoofika mno.

Omino alianzia taaluma yake ya ukufunzi na klabu ya Agro chemicals kabla ya kujiunga na Western Stima .

Alipokuwa katika klabu ya Western Stima Omino atakumbukwa kwa ufanisi wake baada ya kuiwezesha kumaliza katika nafasi ya 6 kwenye ligi kuu ya KPL msimu wa 2016.

Aliandikisha rekodi na kuwa mkufunzi wa kwanza nchini kushinda tuzo ya mkufunzi bora wa mwezi baada ya kuinyakuwa tuzo hiyo mara mbili mfululizo.

Wakufunzi na wachezaji wa wametuma risala za rambi rambi.