Maafisa 7 wa polisi hawajulikani waliko baada ya gari lao kusombwa na mafuriko

unnamed (16)
unnamed (16)
NA NICKSON TOSI

Afisa mmoja wa polisi amefariki huku wengine saba wakiwa hawajulikani waliko baada ya gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na mafuriko eneo la Chemoe kaunti ya Baringo.

Yanajiri hayo huku mratibu wa mipango ya serikali ukanda wa Rift Valley George Natembeya akisema mvua kubwa inayoendelea kunyesha maeneo tofauti ya sehemu hizo, imelemaza shughuli nyingi za uokoaji wa watu.

Natembeya ameongeza kuwa baadhi ya miili ya watu 16, waliofariki italazimika serikali kutumia DNA ili kubaini jamaa zao.

Katika taifa jirani la Tanzania, waziri wa maswala ya katiba na haki Agustine Mahiga amefariki akiwa na miaka 72,

Rais Magufuli amethibitisha kifo kwa kusema Mahiga alifariki alipokuwa anakimbizwa hospitalini Dodoma.