Kariobangi North yageuka kuwa mtaa wa wakimbizi-Tazama

EXT9nzjWAAI_xH-
EXT9nzjWAAI_xH-
NA NICKSON TOSI

Hatua ya serikali kubomoa nyumba katika mtaa wa mabanda wa Kariobangi North imewaacha watu zaidi ya 5,000 kukosa makao na kulazimika kukita kambi katika maeneoa tofauti .

Ni hatua ambayo imekasirisha zaidi mashirika ya kutetea haki za kibinadamu na viongozi ambao wameikashifu serikali kwa kuafikia kuchukuwa hatua hiyo haswa wakati huu ambapo taifa linakabiliana na janga la corona huku mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini ikiangamiza idadi kubwa ya wakenya.

Tazama picha zifuatazo.

Wat

Gavana wa jimbo la Nairobi Mike Sonko hata hivyo ametishia kuelekea mahakama ya ICC na kumshtaki katibu katika wizara ya usalama wa ndani Karanja Kibicho na wenzake kwa kile amesema ni kuwahangaisha wakenya.

Serikali kwa upande wake umejitetea ikisema kuwa nyumba hizo zilijengewa kwa ardhi yake.