Kwendeni kabisa! Madereva 25 waliopatikana na corona kwenye mpaka wa Namanga warudishwa katika mataifa yao

Kenya imewarudisha madereva wa masafa marefu katika mataifa yao baada ya kufanyiwa vipimo na kupatikana na virusi vya corona kwenhye mpaka wa Namanga.

Madereva hao 23 wanatoka katika taifa la Tanzania,Mmoja kutoka taifa la Uganda na mwengine kutoka taifa la Rwanda,taarifa ambazo zimedhibitishwa na wizara ya afya.

Akitoa taarifa za kila siku kwa taifa kuhusiana na virusi hivyo, Dr Rashid Aman alisema Kenya sasa imepata kliniki tamba mbili ambazo zitawekwa kwenye mipaka kuu nchini ili kuwapima madereva kutoka matifa ya ukanda huu.

“We shall soon be receiving mobile laboratories from the East Africa Community to improve disease surveillance...The two fully-equipped laboratories are capable of carrying out Covid-19 testing,” Dr Aman said. “And, hopefully, by next week, one of the two laboratories will be stationed and operational at the Namanga border to facilitate testing of truck drivers at the border point.”'alisema Aman

Kliniki hizo tamba zitatumika kuwapima watu wanaoingiua nchini kutoka Kenya na Tanzania.

Kufikia sasa, Kenya imesajili visa 737, huku watu waliofariki wakiwa 40 na wale waliopona wakiwa 281.