Katika majadala uliodumu kwa saa nne, maseneta 54 walipiga kura ya kumuondoa kindiki kutoka kiti hicho. Waliopinga hoja hiyo ni maseneta saba.
Spika Ken Lusaka aliaziacha nje kura mbili za maseneta waliotaka kupiga kura bila kuwepo baada ya kiranja wa walio wengi Irungu Kang’ata kumshauri kufanya hivyo ili kuepuka pingamizi zozote. Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen alikuwa amepinga kuongezwa kwa kura hizo mbili akisema ni ukiukaji wa katiba.
Awali Kindiki alionyesha masikitiko kwamba chama chake cha Jubilee kilikuwa kikijadili hoja ya kumuondoa ilhali taifa linakabiliwa na changamoto nyingi likiwemo janga la virusi vya corona, hali mbaya ya uchumi na uvamizi wa nzige.
Alisema ni jambo la kusikitisha kwamba anashtumiwa kwa kutomheshimu kiongozi wa chama cha Jubilee rais Uhuru Kenyatta ilhali ana heshima kubwa sana kwa rais.
Amesema wanaomhujumu sio rais Kenyatta wala maseneta.