Uhuru amesema katiba ipo wazi kuhusu muda wa kuhudumu kwa anayeshikilia wadhfa wa urais. Ameongeza pia kwamba hana lengo la kuwa waziri mkuu kama inavyodaiwa.
Uhuru alikuwa akiyajibu maswali ya Katrina Manson wakati wa mkutano uliofanywa kwa njia ya video na Atlantic Council.
Uhuru alisema, “ iwapo kuna kitu ambacho wakenya wanakifahamu kwa uwazi kabisa ni kuhusu mihula miwili ya kuhudumu kama rais. Hilo limekuwa wazi tangu mwaka wa 1992 tulipoanzisha mfumo wa siasa za vyama vingi na hakuna rais ambaye amewahi kuvunja hilo nchini na kamwe sitaki kuwa wa kwanza kufanya hivyo’
Uhuru amesema lengo la mwafaka wa BBI ni kuhakikisha kwamba vizazi vijavyo havikumbani na changamoto zinazolikabili taifa kwa sasa.
" Sina ufahamu wa iwapo kutakuwa na wadhifa wa waziri mkuu katika katiba, Haya sio maswali ambayo watu wameanza kuuliza. Nimekupa mtiririko wa yote ambayo wakenya wanataka yashughulikiwe kama vile nguvu ya kura zao, ugavi wa raslimali na kujumuishwa serikalini’.
Uhuru amesema kando na hayo hajasikia kuhusu masuala mengine yanayoibuliwa na hivyo basi hawezi kuyazungumzia kwani hayamo katika msingi wa BBI