Mbunge mteule Godfrey Osotsi amesema Musalia Mudavadi sio tena kinara wa chama cha ANC na hakuna msukumo kutoka nje ili kuleta mafarakano chamani humo.
Osotsi, amesema Mudavadi na maafisa wengine katika uongozi wa chama hicho wapo afisini kinyume cha sheria kwa sababu muda wao wa kuhudumu umekamilika na kusalia kwao uongozini ni ukiukaji wa katiba ya chama hicho.
“ Kama ilivyo sasa ANC hakina kiongozi wa chama. Mudavadi ameshakamilisha muda wake katika nafasi hiyo, ujumbe huu ni bayana’ amesema Osotsi.
Osotsi alikuwa akijibu madai ya kundi moja la viongozi wa ANC kutoka Migori waliodai kwamba anatumiwa na kinara wa ODM Raila Odinga kuzua mgawanyiko katika chama cha ANC.