Lonna Mwabishi pia alishtakiwa kwa kumshambulia polisi mmoja mwanamke katika kituo hicho. Alishtakiwa kwa kusababisha usumbufu na kuvuruga amani baada ya kuwataja polisi kama ‘watu wafisadi ambao hutumia hongo kufanya ukahaba’.
Mwabishi anashtumiwa kwa kuyatekeleza makosa hayo yote Julai tarehe tatu katika kituo cha Polisi cha Riruta, Nairobi.
Alifikishwa mbele ya hakimu mkuu mkaazi wa kibera Renee Kitagwa ambapo alikana mashtaka dhidi yake. Inadaiwa alimshambulia afisa wa polisi Walloce Bundi.
Hata hivyo alikanusha mashtaka yote dhidi yake na kusema kwamba ni polisi hao ndio waliomshambulia. Amesema polisi walipendekeza mashtaka hayo dhidi yake ili kuficha ukatili wao. Aliachiliwa kwa bondi ya shilingi 50,000 au dhamana ya shilingi 20,000 pesa taslimu.
Kesi hiyo itatajwa Julai tarehe 21.