Mashakani: Mahakama yakataa kuzuia hoja ya kumuondoa Ngilu afisini

Ngilu
Ngilu
Gavana wa Kitui  Charity Ngilu amepata pigo baada ya mahakama kukataa kuzuia kuwasilishwa kwa hoja ya kumuondoa afisini.

Ngilu  alikuwa amewasilisha kesi kortini Juni tarehe 24 akitaka kupata maagizo ya kuwazuia wawakilishi wa kaunti dhidi ya kuuwasilisha bungeni mswada wa kumuondoa mamlakani.

Jaji Welson Korir  siku ya Alhamisi amesema  ombi la Ngilu halikuwa na msingi wa kutosha wa kushurutisha kutolewa kwa maagizo aliotaka

Korir pia amesema  ombi hilo liliwasilishwa Nairobi na sio  katika kaunti ya Kitui.

Jaji ameongeza kwamba  ni muhimu kwa wakaazi wa kaunti iliyoathiriwa waweze kufika mahakamani kufuatilia kikao kinachoendelea kuhusu uongozi wa kaunti yao.