Omar Lali, aliyekuwa mpenzi wa mrithi wa Keroche marehemu Tecra Muigai aachiliwa huru

Omar Lali
Omar Lali

Omar Lali aliyekuwa mpenzi wa Tecra Muigai mrithi wa kampuni ya Keroche Breweries aliachiliwa huru siku ya Alhamisi baada ya mkurugenzi wa mashataka ya umma DPP kusitisha kesi ya mauaji dhidi yake na kuomba pafanyike uchunguzi wazi kuhusu kifo cha Tecra.

Habari zingine;

Lali mwennye umri wa miaka 54, alikuwa ashtakiwe kuhusiana na kifo cha Tecra baada ya DPP kutathmini ripoti zote za uchunguzi wa kifo cha mwanamke huyo zikiwemo ripoti za upasuaji wa mwili wake, rekodi za simu, stakabadhi zingine na taarifa za mashahidi.

Msimamizi wa mashtaka Eddie Kadebe na mwenzake Zakaria Kiongo walikuwa wamesema kwamba kulikuwepo ushahidi wa kutosha kumshtaki Lali kwa mauaji.

Habari zingine;

Tecra bintiye afisa mkuu mtendaji wa Keroche Tabitha Karanja, alifariki mwezi Mei mwaka huu kwa kile kiliripotiwa kuwa tukio la ajali.

Alipata jeraha la kichwa baada ya kuanguka katika nyumba walimoishi na Lali mjini Lamu.