‘Babu wa loliondo yupo?’ Nyota Ndogo ataka kuwaangamiza waliomwibia katika mkahawa wake

Msanii   Nyota Ndogo  maajuzi alifungua mkahawa wa ‘Nyota Ndogo Jikoni’.

Lakini kwa bahati mbaya, mwanamuziki huyo anasema wezi walivamia hoteli yake na kuiba vitu ikiwemo  chapati tano, mafuta ya kupikia na gesi yake. Alitumia mitandao ya kijamii kueleza  mkosi huo.

“LEO TUMEINGIA KAZINI ASUBUI TUMEKUTA VITI NJE KIFULI KIMEVUNJWA. SASA VILIVYOIBIWA NDIZI, CHAPATI ZILIKUA ZIMEBAKI TANO, GESI YANGU, MAHARAGE KILO MBILI BOX LA MAFUTA YA SAMLI YANI MAFUTA YA MGANDO FRIZA WAMEJARIBU KUITOA WAMESHINDWA.

Aliongeza

‘HIVI YULE BABU LOLIONDO YUPO JAMANI TUWAKUTE WAIZI MLANGONI HASUBUI. MTUNGI MZIMA WA LITA MBILI WOTE UMEENDA NA NIMEFANYA SHOPPING JANA TU MPYA MUNGU AWAONA NITARUDISHA FRIZA HOME LEO YANI DUH MTU ATAONA NIKIDOGO BUT KWA ANAE AMKA 4AM KUANZA KUPIGWA NA MOSHI UNAMUIBIA AMANI NAYO HUTAIJUA”

Nyota  amekuwa akiitangaza biashara yake mitandaoni na wasanii wenzake wa pwani wamekuwa wakimpiga jeki sana kwa sababu biashara yenyewe iko huko.