'Omar alituambia tusafishe damu,'Mtunza nyumba aeleza nyakati za mwisho za Tecra Muigai

EYMDMzeXsAA50Jn-1
EYMDMzeXsAA50Jn-1
Mtunza nyumba katika jumba la Jaha Guest House ambapo Tecra Muigai na mpenzi wake Omar Lali alikokuwa wanaishi, alisema kuwa alipata damu kwenye ngazi ya nyumba hiyo.

Aliwaambia wachunguzi kuwa alipokuwa ananenda kusafisha nyumba hiyo siku hiyo ya tukio saa moja unusu, hakupata mtu yeyote katika jumba lao ilhali aliona damu kwenye ngazi kuelekea katika ghorofa ya pili.

Simu na kompyuta ya mkononi ya mwanawe mkurugenzi mkuu wa kapuni ya mvinyo ya Breweries zilikuwa kwenye kiti ilhali simu ya mpenzi wake ilikuwa imezimwa.

Mtunza nyumba huyo alisema kuwa aliripoti kisa hicho kwa maneja wake, bwana Lali aliwaambia wasafishe damu hizo na nyumba yote kwa jumla 'Kwa maana ilikuwa tukio dogo'.

Tecra Muigai aliaga Mei mwaka huu huku ikidaiwa ilikuwa ajali, aliaga kutokana na majeraha aliopokea kwenye kichwa chake baada ya ajali hiyo.

Alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Omar lakini Uhusiano wao ulifahamika wakati wa kifo chake.