Mara ya mwisho kumuona aling'ang'ana kutabasamu,' Abel Amunga amuomboleza muewe Ruth Matete

Muigizaji Abel Amunga na baba wa msanii Ruth Matete amemsifu mwendazake John kwa kuwa mwanamume wa kipekee hadi siku ya pumzi yake ya mwisho.

Huku akimuomboleza katika hafla ya mazishi yake Amunga alisema,

"Bado nina nguvu kwa maana huyu mwanamume amelala hapa alikuwa na nguvu adi pale aliaga dinia."

John amezikwa hii leo katika makaburi ya Lang'ata huku watu tofauti wakihudhuria sherehe za mazishi hayo;

"Nakumbuka pale katika hospitali kuu ya Kenyatta nilipoenda kumtembelea aling'ang'ana kutabasamu nami nikatabasamu pia mwanangu, rafiki yangu na hata muombaji wangu

Nakumbukka kuna wakati nilikuwa mgonjwa maututi, John na Ruth walikuja nyumbani kwangu na kuniombea Mungu alithihirisha mambo mengi lakini siku iliyofuata nilikuwa nimepona."