'Walikuwa wamevalia kama mapepo,' Nyota Ndogo afichua wezi waliotaka kumuibia tena

Nyota
Nyota
Siku chache baada ya wezi kuingia katika hoteli yake na kuiba bidhaa msanii nyota ndogo ameeleza jinsi wezi hao walivyokuwa wamevalia kama vizuka yaani mapepo.

Wezi hao walijifanya kuwa mapepo huku wakimuacha mlinzi na hofu nyingi.

"Leo nimecheka sana,wezi walijipaka mafuta machafu kweyr nyuso zao na kuvunja katika hoteli yangu bila ya kujuwa kuwa mlinzi alikuwa kwenye doria

Wakati mlinzi huyo alipowaona alishtuka na kufikiria walikuwa mapepo karibu apige nduru, lakini wakati aliwatazama vyema aligundua walikuwa ni binadamu

Nilishika kisu na wezi hao walikimbia, nitaanza kusoma kwa makini albadiri za watu ilhali haijakubaliwa lakini wakizidi nitajilinda aj." Nyota Alisema.

Awali nyota Alieleza jinsi bidhaa za hoteli yake ziliibiwa,

"LEO TUMEINGIA KAZINI HASUBUI TUMEKUTA VITI NJE KIFULI KIMEVUNJWA.SASA VILIVYO IBIWA NDIZI CHAPATI ZILIKUA ZIMEBAKI TANO GESI YANGU MAHARAGE KILO MBILI BOX LA MAFUTA YA SAMLI YANI MAFUTA YA MGANDO.

FRIZA WAMEJARIBU KUITOA WAMESHINDWA HIVI YULE BABU LOLIONDO YUPO JAMANI TUWAKUTE WAIZI MLANGONI HASUBUI.MTUNGI MZIMA WA LITA MBILI WOTE UMEENDA.

NA NIMEFANYA SHOPPING JANA TU MPYA MUNGU AWAONA NITARUDISHA FRIZA HOME LEO YANI DUH MTU ATAONA NIKIDOGO BUT KWA ANAE AMKA 4AM KUANZA KUPIGWA NA MOSHI UNAMUIBIA AMANI NAYO HUTAIJUA."