MCA’s wa Nairobi waapa kumtimua Spika Elachi

mcas
mcas
Baadhi ya wawakilishi  wa  bunge la kaunti ya Nairobi wameanzisha mchakato mwingine wa kumuondoa afisini spika wa bungela kaunti hiyo Beatrice Elachi .

Wawakilishi 51 kati ya 107  tayari wamesaini  waraka malaum wa kumtimua afisini Elachi  nan i sahihi 42 tu zinazohitajika ili kufanikisha hoja ya kumtimua Elachi ambaye wamekuwa wakijaribu kumuondoa madarakani tangu mwaka wa 2018.

Wawakilishi hao  wanamshtumu Elachi kwa uongozi unaozua mgawanyiko na kutowaheshemu wanaoshikilia nyadhifa za   uongozi katika bunge la kaunti .

“ Elachi anaongoza bunge kw anjia inayozua mgawnayiko ,ufisadi  na mwenye makaovu ya kale kulipiza kisasi’ amesema naibu  kiranja  wa walio wemngi   Waithera Chege .

Mwakilishi wa eneo la Utalii Wilson Ochola  amemshtumu Elachi kwa kutowaheshimu wawakilishi wa kaunti  na kuwakandamiza wale wanapopinga maamuzi yake .

Mwakilishi wa wadi ya Hamza  Mark Ndung’u  pia amemlaumu Elachi kwa kuleta mgawnayiko kati ya serikali ya kaunti ya  Nairobi na  Mamlaka ya kusimamia Jiji la Nairobi .

Amesema  Elachi  ana mazoea ya kuyataja majina ya rais Kenyatta na Raila Odinga  ili kuwashurutisha wawakilishi wa kaunti kupitisha  maamuzi yake ambayo wengi wanayapinga .