Model aliyehusishwa na Diamond Platnumz akana kwamba ni mpenzi wake

Model Jihan Dimack amabye amekuwa akihusishwa na uwezekano kwamba yupo katika uhusiano na msanii wa Tanzania Diamond Platinumz amejitokeza kueleza wazi kwamba hayupo katika uhusiano kama huo na Diamond .

Mamake Diamond ndiye aliyezua uvumi huo alipomposti kipusa huyo katika instagram  na uvumi  huo ukakomaa na hata pakatokea habari kwamba huenda wawili  hao walikuwa wakipanga kufanya harusi .

Katika mahojiano na  Sky Walker ma Creez Favors  wa SnS  model huyo alijitenga na uvumi huo .

Amesema yeye na Diamond wanajuana kwa sababu wapo katika fani moja na hamna la ziada  na  wao ni marafiki tu

Pia aliongeza kwamba hana mpango wa kuolewa hivi karibuni .

“It’s very crazy,  Napata hata simu kutoka Urusi watu wakiniuliza kwamba  mbona sikusema kwamba naolewa  na mwanamuziki staa . na sijui mbona kila wakati nikienda kwenye hizi hafla watu wanaweka na mtu mwingine kisha najipata nikitrend’

Alikataa kutoa jibu la moja kwa moja alipoulizw aiwapo anaweza kuzingatiwa kuwa  katika mahusiano ya kimapenzi na  Diamond .

“ kwa kweli siwezi kusema lolote kuhusu hilo kwa sababu haijawahi kufika kiwango hicho na ikifanyika basi kila mtu atajua  kwani sidhani anaweza kutaka uhusiano huo uwe wa siri .ni vigumu sana kwangu kuw ana mtu ambaye  yupo machoni pa umma kwa sababu napenda mambo yangu kuwa chini chini  lakini huwezi kujua’