Niliumizwa:Mbosso aeleza jinsi aliumia moyo wake kwa ajili ya mapenzi

Mbosso
Mbosso
Msanii wa bongo Mbosso amesema sababu huwa anatoa vibao vyenye mapenzi tele ni kwa sababu alipenda na wakati huo akaumizwa moyo wake.

Msanii huyo alisema hayo wikendi iliyopita huku akisema kuwa kuna wimbo atakao utoa ambao unaelezakuhusu safari yake ya mapenzi.

"Naogopa kuumiza moyo wa mtu husiwahi danganya unapenda mtu ilhali haumpendi kwa maana najua jinsi mtu husikia wakidanganywa na kuumizwa

Nimeumizwa awali huwa naogopa kuumiza mtu ambaye ananipenda ni afadhali niambie mtu ukweli kuliko kumdanganya, unastahili kutumia nguvu nyingi kulinda uongo wako kwa maana uongo huo utaukumbuka kesho ili usiseme maneno ambayo yanachanganya maelezo yao ya awali." Alisema Mbosso.

Alisema kuwa alipokuwa anatoa kibao chake cha 'nipepee alikuwa kwenya mahabara ya mapenzi  kupindukia lakini alipokuwa anatoa kibao chake cha 'Nadekezwa alikuwa ameumizwa moyo.

Mbossso amejiandaa kuzindua na kutoa albamu mpya huu mwaka.