Wakati wa kurekebisha katiba iwe bora ni sasa-Uhuru

Rais Uhuru Kenyatta amesema wakati umewadia wa kuorekjebisha katiba .Rais amesema licha ya katiba ya sasa kuwa bora mkuna umuhimu wa kuirekebisha katiba ili iweze kustahimili muda na changamoto zote zijazo .

Rais Kenyatta amezitaja katiba za hapo awali kama zilzioundwa kuzuia ama kumaliza uhasama lakini haziwezi kutegemewa kuliboresha taifa asiku zijazo .

Katika kinachoonekana kama hatua ya kuwatayarisha wakenya kwa kura  ya maoni  kuhusu katiba mrais amesema katiba inafaa kuchukuliwa kama chombo cha kuboreshwa kwa lengo la kuimarisha  utawala na utoaji wa huduma kwa wakenya. Kuna mjadala kwa sasa kuhusu iwapo kura ya maonia kuirekebisha katiba inafaa kuandaliwa kwanza kabla ya uchaguzi .

viongozi wanaounga mkono mchakato wa BBi wamekuwa wakiitisha kuandaliwa kwa kura ya maoni kuirekebisha katiba huku wanaopinga mchakato huo wakikosoa pendekezo la kuirekebisha katiba . Katiba ya sasa imekuwa ikitumiwa kwa miaka kumi sasa tangu ilipoanza kutekelezwa mwaka wa 2010.

Wanaopinga kurekebishwa kwa katiba wanadai ni njama  ya kuanzisha mfumo wa utawala utakaoongeza nafasi za uongozi wa kurejesha tena nafasi ya waziri mkuu na manaibu wake .