Akizingumza na wahubiri wa kiislamu katika hoteli ya Pride inn huko Shanzu Mombasa Ruto amesema wanachama wa Jubilee wanaompigia debe mgombeaji mwingine wanakiuka msimamo wa chama hicho .
" Iwapo mgombeaji wako yuko Orange House mnafanya nini Jubilee? Nendeni Orange House!’ Alisema Ruto
Alikuwa akiwajibu wale waliomtaka ajiuzulu kama naibu kinara wa chama na Naibu wa Rais
Naibu mwenyekiti David Murathe na mbunge wa Nyeri mjini Ngunjiri Wambugu ni miongoni mwa viongozi waliomtaka Ruto kujizulu wakisema anakiuka kila msimamo wa mkuu wake Rais Uhuru Kenyatta .
Ruto aliwataka wafuasi wake wanaoteswa kwa sababu ya kumuunga mkono kusalia na ukakamavu .
Alisema chama cha Jubilee kina wanachama milioni nane na kinawahudumia wakenya milioni 45 hivyo basi hakuna anayefaa kumtisha yeyote .