Aisha Jumwa aachiliwa huru kwa dhamana ya millioni mbili

jumwa
jumwa
Baada ya mbunge Aisha Jumwa kujisalimsha kwa polisi mnamo Agosti,30, na kuwaambia wanahabari kuwa ataenda mbele ya mahakama Jumatatu hatimaye ameachiliwa kwa dhamana ya shillingi millioni mbili.

Jumwa anakabiliwa na mashtaka ya ubadhirifu wa KSh.19 milioni pesa za Maendeleo ya eneobunge (CDF).

Anatuhumiwa kupokea pesa kwa njia ya ulaghai kupitia Multserve Contractors Limited, kampuni iliyopewa zabuni ya kujenga Ofisi ya Elimu ya Kaunti ndogo ya Malindi.

“Multserve Contractors Limited ilipokea KShs. 19,002,000.00/=, katika pesa hizo KShs. 2,500,000.000/= zinadaiwa kutumwa kwa Mhe. Aisha Jumwa Karisa Katana akiwa Mbunge wa Malindi. Hii ni kinyume cha sheria,” Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji alisema. 

Kulingana na DPP, Jumwa alipokea pesa hizo, zilizotokana na jinai, kupitia malipo ya polepole ya ununuzi wa nyumba kwenye Barabara ya Argwings Kodhek jijini Nairobi.

Hku akiwa mbele ya hakimu wa mahakama ya Mombasa Ednah Nyaloti, Aisha aliachiliwa huru kwa shillingi millioni mbili huku walioshatakiwa naye wakiachiliwa kwa shilingi 500,000.