Mkuu wa NMS Badi Kuhudhuria mikutano ya baraza la mawazi baada ya kula kiapo cha kuweka siri

badi
badi
Mkurugenzi mkuu wa  usimamizi wa Mamlaka ya Nairobi  Mohammed Badi  atakuwa akihudhuria mikutano ya baraza la mawaziri baada ya kula kiapo cha kuweka siri .

Kupitia taarifa iliyotumwa siku ya alhamisi ,Ikulu imesema kwamba rais alishuhudia hafla ya kuapishwa kwa Badi  kama inavyohitajika na wote wanaohudhuria mikutano ya baraza la mawaziri  au wanaoshughulika na tarataibu za   uendeshaji wa serikali .

Msemaji  wa Ikulu Kanze Dena amesema  kuanzia sasa Mkuu huyo wa NMS  atakuwa akihudhuria mikutano ya baraza la mawaziri na kamati zake  kwa mujibu wa agizo la rais la tatu la mwaka wa 2020 .

Hafla hiyo iliandaliwa alhamisi kabla ya mkutano wa baraza la mawaziri kufanyika