" Naelekea kukagua barabara moja hapa chini ambayo tunajenga na itaunganisha Naiorbi kupitia Kiambu hadi Murang’a kisha ifike Nyeri… niliwaambia mimi haja yangu ni kazi ..’ amesema rais
" Hata kama umri wangu ni mdogo sina tatizo na kwenda nyumbani ili mradi watu waone kazi ambayo nimefanya . hawa wajinga wanaozunguka wakitoa matusi ,waambie watusi mama zao na waachane na wangu..’
Uhuru ambaye alikuwa kizungumza kwa lugha ya kikuyu amesema viongozi wanafaa kushirikiana kuleta umoja na Amani .
".. Sitajiruhusu kuzungumza kwa hamaki kwa sababu nawataka wakenya kuishi pamoja kwa Amani’
" taifa litasalia kuwepo lakini sisi kama watu hatutaishi milele’
Matamshi hayo ya rais yanajiri baada ya mbunge wa Emurua Dikiir Johanna Ng’eno na wa kapsrete Oscar Sudi kurekodiwa wakizingumza matamshi ambayo yalionekana kumlenga rais Kenyatta na familia yake . Ng;eno baadaye alikamatwa na ameachiliwa leo na mahakama kwa dhamana ya shilingi milioni 1
Baadhi ya viongozi wamejitokeza kutoa onyo dhidi ya mtindo wa kutumia lugha mbaya nay a uchochezi inayotishia Amani ya nchi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022