cha Musalia Mudavadi baada ya kusema kulikuwa na haja kwake kuondoka ili kutoa nafasi ndani ya chama hicho .
Kupitia taarifa siku ya jumatatu Owalo amesema Kenya inahitaji kiongozi thabiti mwenye historia ya uongozi wa kuwahusisha wote na anayewajali watu .
Amesema baada ya kutafakari hali na wagombeaji wa urais mwaka wa 2022 amefanya uamuzi wa kujiunga na kundi la ‘Hustler’ .
" Pia nitamaliza safari a Bill Ruto mwaka wa 2022’ amesema kupitia taarifa yake.
Owalo pia amesema kwamba hajaona sababu ya katiba kurekebishwa . Ameshangaa haraka iliyopo kuifanyia katiba mageuzi kwani hapana haja au cha msingi kinachohitaji kushughulikiwa kwa dharura .
" kwa maoni yangu tatizo letu sio katiba bali kukosa kuitekeleza katiba kikamilifu na kutumikia matakwa na azma za wananchi’ amesema Owalo katika taarifa yake hiyo .
" Jambo la kuzua wasi wasi ni kwamba kuna kundi ambalo linalenga kuwarundika wakenya katika makundi ya makabila yao kwa lengo la kushinda maamlaka’ ameongeza Owalo .
Owalo amesema ili kuiokoa Kenya kutoka mgogoro wa sasa wa kiuchumi na utata wa kisiasa wakenya wanafaa kuungana kwa pamoja kutafuta dhamira ya kuwaunganisha bila kujali makabila yao bali kwa maslahi ya taifa zima