Wafanyibiashara katika eneo la Nairobi Railways club wameamkia hasara baada ya biashara zao kubomolewa usiku . Maamlaka zilitekeleza ubomoaji huo usiku wa kuamkia jumatano baada ya wafanyibiashara hao kupewa notisi ya kuondoka ili kutoa nafasi ya ujenzi wa barabara mpya ya Nairobi Express Way.
Vikosi vya maafisa wa polisi vilikuwa vimepiga kambi katika eneo hilo na ni wafanyikazi wa hoteli pekee walioruhusiwa kuingia ndani .Mkuu mmoja wa polisi alisema maelezo Zaidi kuhusu tukio hilo yangepatikana katika makao makuu ya shirika la Reli .
Pharis Ngotho, kaimu afisa mkuu mtendaji wa mpango mafaai ya kustaafu wa wafanyika wa shirika la Reli alikuwa ametuma arifa ya kuwashauri wafanyibiashara katika eneo hilo kuondoa bidhaa zao kwa sababu ardhi hiyo ilikuwa inachukuliwa na serikali kwa lazima kufanikisha mradi huo wa barabara .
Miongoni mwa walioathiriwa na ubomoaji huo ni wauzaji wa magari