Maseneta walalamikia kukatiliwa kwa misuada yao 13 na bunge la kitaifa

lusaka
lusaka

Taarifa ya Julius Otieno

Malumbano mapya ya ubabe baina ya bunge la kitaifa na seneti yamezuka tena kuhusiana na misuada.

Maseneta wanapinga kukataliwa kwa jumla ya misuada 13 na wabunge hatua ambayo imefufua tena uhasama baina ya mabunge hayo mawili.

Maseneta walilalamikia kiwango ambacho misuada yao inakataliwa na bunge la kitaifa kwa misingi kwamba ni misuada ya kifedha.

“Inauma sana. kutayarisha misuada hujumuisha mashauriano, wadau...kuna wataalam wanao tayarisha misuada hii na kisha unaambiwa kwamba imekataliwa,” Seneta Sylvia Kasanga alisema.

Seneta huyo maalum ni mwenyekiti wa kamati maalum ya seneti kuhusu hali ya Covid-19 nchini.

Msuada wa kudhibiti majanga, uliotayarishwa na kamati hiyo unaotoa muongozo wa kisheria kuhusu kudhibiti virusi vya corona na majanga mengine siku za usoni, ni miongoni mwa misuada ambayo imetupwa na bunge la kitaifa.

Kiranja wa wachache katika seneti Mutula Kilonzo Jr alisema kwamba seneti imepoteza sana na kumtaka spika Kenneth Lusaka kuzungumza na mwenzake wa bunge la kitaifa Justin Muturi kupata suluhu kwa suala hili.

“Kuna misuada 13 ikiwemo yangu ambayo imepuuzilia mbali. Nilitayarisha msuada wangu mwaka 2017 na umetupwa kwa sababu ni msuada wa kifedha,” alisema.

Soma habari zaidi hapa;