Rais wa Marekani Donald Trump na mkewe wapatikana na corona

Rais wa Marekani Donald Trump na mkewe Melania Trump kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya twitter walitangaza ya kwamba wamepatikana na maambukizi ya virusi vya corona.

Alitangaza haya baada ya mmoja wa wandani wake aliyefahamika kama Hope Hicks amepatikana na virusi hivyo.

"Usiku huu mke wangu na mimi tumepatikana na virusi vya corona,tutaanza karantini na kuanza matibabu haraka iwezekanavyo

tutapitia haya pamoja." Aliandika Trump.

https://twitter.com/realDonaldTrump/status/1311892190680014849

Habari hizo pia zilidhibitishwa na memo ilioandikwa na Sean Conley ijumaa asubuhi huku akisema kuwa wawili hao wamepatikana na corona na watkuwa karantini katika white house.

"Usiku wa leo nimepokea dhibitisho kuwa rais Donalf Trump na mkewe Melania Trump wamepatikana na corona ,rais na mkewe kwa sasa wamo kati hali dhabiti na watasalia white house huku wakipokea matibabu."Conley Sliandika.

Kutoka kwetu wanajambo tunawatakia afueni ya haraka, ama kweli hawakukosea waliposema virusi hivi havibagui tajiri,maskini, kiongozi na mwananchi wa kawaida.

Pia mkewe rais althibitisha habbari hizo na kusema kuwa ameahirisha mipango yake yote kwa ajili ya virusi hivyo.