'Nitakapo maliza kazi yangu kama rais nitaoa bibi wa pili,'Rais Magufuli

Rais Wa Tanzania, Magufuli
Rais John Pombe Magufuli anafahamika sana kwa ujasiri wake mnamo JUmamosi aliwaacha wananchi kwa kicheko na tabasamu baada ya kufichua endapo atakamilisha kazi yake ya urais atamuoa mke wa pili

Magufuli ambaye alikuwa anafanya kampeni nchini Ugunja alifanya mzaha kuwa ameona mambo mazuri maeneo hayo,wanawake warembo na yuko na mipango ya kumpendekeza mmoja.

Magufuli ambaye anawania kiti cha urais kwa mara ya pili alisema kuwa siri ya kuishi kwa muda mrefu ameitoa kwa aliyekuwa rais wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi ambayo ni kuoa wake wengi.

"Mnamjua mzee Mwinyi ambaye sasa ana miaka 96 alinipa siri ya kuishi kwa muda mrefu ni kuwa na wake wawili, nina mmoja lakini nitakapo maliza kazi yangu kama rais nitatafuta mke wa pili kutoka Ugunja

Nimeona mambo mazuri huku." Aliongea Maghufuli.

https://twitter.com/ccm_tanzania/status/1312307570531475456

Haya yanajiri miezi chache baada ya rais huyo akifanya kampeni katika maeneo ya Kisarawe aliwashauri wanaume waamke na kumuoa Jokate Mwegelo mmoja wa maafisa wa serikalini.