• Oparanya amesema serikali za kaunti zinafaa kushauriwa kuhusu usajili
• Ameongeza kwamba utekelezaji wa UHC ni jukumu la serikali kuu na za kaunti
Mwenyekiti wa baraza la magavana Wycliffe Oparanya ameitaka wizara ya afya kukomesha usajili unaoendela wa NHIF katika kaunti .
Hii ni baada ya kaunti kugundua kwamba usajili huo unaendeshw akatika kaunti zao bila magavana kujulishwa .
Mojawapo ya ajenda kuu za rais Uhuru Kenyatta ni utekelezwaji wa mpango wa kutoa huduma za bure za matibabu kwa wananchi wote .
Mpango huo wa UHC sio tu jukumu la serikali kuu bali unafaa kutekelezwa kwa ushirikiano na serikali za kaunti .
“ Komesheni mpango huo wa usajili wa NHIF… kukosa kushauriana nasi na uksoefu wa uwazi katika usajili huo ni jambo ambalo litazaa kutoaminiana’ Oparanya amesema
Kupitia taarifa siku ya jumanne Oparanya amesema usajili wa NHIF katika kaunti haufai kufanywa bila kauinti kuhusishwa.
" Utaratibu huo muhimu unafaa kufanywa na vitengo vyote vya serikali baada ya kukubaliana kuhusu jinsi ya kuendesha usajili huo na namna ambavyo mradi mima wa UHC utakavyofanikishwa’ ameongeza.