'Kazi nimefanya!' Khaligraph na mkewe Georgina watarajia mtoto wa pili

OG ni OG! Khaligraph na mkewe Georgina Muteti wametangaza kuwa wanatarajia mtoto wa pili, hivi karibuni.

Kupitia mtandao wake wa Instagram, Khaligraph ambaye ameteuliwa katika tuzo za BET, alitangaza kuwa amekuwa akifanya kazi katika nyanja zote za kimaisha, na matokeo yanajionesha.

"Omollo amekuwa akifanya kazi zaidi katika kila uwanja, OG lazima ataheshimika, Rada Safi.
"

(Omollo Has been OverWorking in Every Field, The OG has to be Respected, Rada Safi, The Lwanda Magere Legacy 🔥🔥)

 

Mwezi Juni mwaka uliopita, Khaligraph na Georgina walikaribishwa kifungua mimba wao, mtoto wa kike kwa jina, Amina Jones Ouko duniani.

Mashabiki, jamaa na marafiki walizipokea habari zile kwa furaha kuu huku wakiwapongeza wapenzi hao.

Tazama baadhi ya jumbe ambazo alipokea Khaligraph:

Betty Kyllo: Overworking

Bienaimesol: Father of a great nation

Official Wayne: Yaani ni Father figure kila sekta

Official Mwaniki: God bless you and your family

Tazz: congratulation giant OG🦅 

Tunampongeza sana bwana Khaligraph na mkewe bi Georgina.